AU inajaribu kupatanisha Libya

Ujumbe wa Umoja wa Afrika, AU, unawasili Libya leo kujaribu kusitisha vita huku mapigano yanaendelea nchini.

Haki miliki ya picha Getty Images

Ma-rais wa Afrika Kusini, Mauritania, Mali na Congo wanakwenda Tripoli ambako wanatarajiwa kukutana na kiongozi wa Libya, Colonel Gaddafi.

Tena watakwenda Benghazi kuzungumza na waakilishi wa vuguvugu la wapiganaji.

Ujumbe huo wa AU umetoa wito kuwa uhasama umalizwe haraka, na umependekeza kipindi cha mpito ambapo mabadiliko ya kisiasa yanaweza kutekelezwa nchini Libya.

Msemaji wa wapiganaji alisema mapendekezo yoyote yale ni lazima yamtake Kanali Gaddafi na watoto wake kuondoka madarakani.