Viongozi wa upinzani Uganda wakamatwa

Polisi nchini Uganda imewakamata viongozi watatu wa vyama vya upinzani nchini humo kwa kushiriki maandamano ambayo wanasiasa waliyasema ya kupinga kupanda bei za bidhaa muhimu na pia uchumi wa taifa kusimamiwa vibaya.

Haki miliki ya picha Majimbo Kenya
Image caption Kiiza Besigye

Miongoni mwa hao ni Dr Kiiza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change- FDC- Nobert Mao wa chama cha Democratic Party-DP pamoja na Ken Lukyamuzi wa Conservativer Party –CP.

Kiongozi wa chama cha FDC Dr Kiiza Besigye alikamatwa katika barabara moja mjini Kampala ambapo alikuwa anatembea kwenda kazini. Wakati akitembea kwa miguu alizingirwa na polisi na kukataliwa kuendelea. Nae alikaa chini kando mwa barabara.

Baada ya kukaa mahali hapo kwa muda wa saa bili na kuwauliza askari polisi wanamshikilia kwa makosa gani, Besigye alibebwa na kutupwa ndani ya gari lililokuwa hapo na kupekwa kituo cha polisi cha Kasangati.

Besigye amefunguliwa mashtaka ya kuchochea ghasia na pia kutatiza uasafiri wa magari barabarani. Baadae aliachiliwa kwa dhamana na kupewa onyo la kuzingatia amani kwa kufuata sheria.

Lakini yeye anasemekana atarudia kutembea siku ya Alhamisi. Kiongozi mwingine wa upinzani Nobert Mao inasemekana alikuwa ndio anapeklekwa mahakamani kusomewa mashataka. Ken Lukyamuzi yeye alipelekwa nyumbani kwake na kupewa kifungo cha nyumbani.