Man United na Chelsea, Rafael wasiwasi

Beki wa pembeni Mbrazil Rafael ndiye pekee anatiliwa mashaka kwa kikosi cha Manchester United huenda asicheze katika mpambano wa siku ya Jumanne wa robo fainali ya Ubingwa wa Ulaya mkondo wa pili dhidi ya Chelsea.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rafael kutocheza na Chelsea

Ingawa alitangazwa yupo imara siku ya Jumamosi, Rafael alizuiwa kukimbia na kuuchezea mpira pamoja na kikosi kizima katika mazoezi siku ya Jumatatu.

Alitolewa nje ya uwanja kwa machela katika mchezo wa kwanza, Manchester United waliposhinda 1-0 wiki iliyopita katika uwanja wa Stamford Bridge.

Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti, wakati huo huo amesema kikosi chake chote kizima kwa mara ya kwanza msimu huu.

Yossi Benayoun na Alex wamekwishapona tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, wote walicheza katika mchezo dhidi ya Wigan, wakiwa wachezaji wa akiba.

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson, amesema Rafael kuumia kwake ni kidogo na hakuvunjika mfupa wowote.

Wayne Rooney na Rio Ferdinand hawakucheza mchezo dhdi ya Fulham siku ya Jumamosi kwa sababu ya kufungiwa na kuumia - lakini watacheza mpambano wa Jumanne.

Benayoun, ambaye alicheza kwa muda wa dakika 45, Chelsea walipowalaza Wigan 1-0 mwishoni mwa wiki, ukiwa mchezo wake wa kwanza tangu tarehe 22 mwezi wa Septemba, alieleza katika mtandao wa Chelsea: "Siko tayari kucheza dakika zote 90, lakini nitacheza kwa bidii na kuisaidia timu yangu iwapo meneja ataamua kunipanga.