Huwezi kusikiliza tena

CCM Tanzania chatangaza safu mpya

Chama tawala nchini Tanzania CCM kimetangaza safu mpya ya uongozi baada ya kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi katika ngazi ya sekretariat na kamati kuu. Hatua hii inafuatia kujiuzulu kwa mara ya kwanza katika historia kwa kamati nzima ya awali. Katika mabadiliko hayo mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete amemteua Wilson Mkama kuwa katibu mkuu mpya wa chama hicho nafasi iliyoachwa na Bw Yusuph Makamba.

Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (bara) John Chiligati, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa Mwigulu Mchemba, Katibu wa Organaizesheni wa CCM Taifa, Asha Abdallah Juma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye.

Zawadi Machibya alizungumza na Nape Nnauye kutaka kujua nafasi ya CCM baada ya mabadiliko hayo na akiwa kijana, binafsi ameipokeaje nafasi hiyo.