Uganda:Hakuna ruhusa kuandamana,polisi wasema

Kizza Besigye Haki miliki ya picha Reuters

Polisi nchini Uganda wametoa onyo kwa upinzani wasiandamane tena.Viongozi wa upinzani wamepanga kuandamana tena siku ya Alhamisi kwa kile wanachosema kuwa ni kupinga kupanda bei za bidhaa muhimu na pia uchumi wa taifa kusimamiwa vibaya.

Akizungumza na BBC mkuu wa polisi Meja Jenerali Kale Kayihura amesema upinzani ulitakiwa kutoa ilani ya kufanya maandamano hayo mapema na wala siyo kuamua tu ghafla.

Kiongozi wa chama cha FDC Dr. Kiiza Besigye anasema kuwa katiba inamruhusu kutembea kwa miguu kwenda kazini kwa kuwa ni uamuzi wake binafsi kama raia wa Uganda.

Siku ya Jumatatu viongozi wa upinzani akiwemo Besigye na Nobert Mao walikamatwa na polisi walipojaribu kutembea kwa miguu lakini baadaye wakaachiliwa kwa dhamana.