Stoke City yatinga fainali ya FA

Stoke City imeichapa Bolton mabao 5-0, katika nusu fainali ya kombe la FA kwenye uwanja wa Wembley na kujihakikishia nafasi ya kucheza fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Image caption Kenwyne Jones

Magoli ya Stoke yamefungwa na Matthew Etherington, Robert Huth, Kenwyne Jones na Jon Walters.

Mpaka mapumziko Stoke walikuwa mbele kwa mabao 3-0.

Mara ya mwisho kwa Bolton kucheza fainali ya kombe la FA ilikuwa mwaka 1958.

Stoke City sasa itakutana na Manchester City iliyoizaba Manchester United katika nusu fainali nyingine.