Real Madrid yashinda Copa Del Rey

Real Madrid imeichapa Barcelona bao 1-0 na kunyakua kombe la kwanza katika msimu wa soka nchini Uhispania.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Cristiano Ronaldo

Bao pekee la Cristiano Ronaldo katika dakika za nyongeza ndio limeipa Real ushindi huo.

Real Madrid na Barcelona zitakutana tena mara mbili katika mchuano wa kuwania kucheza nusu fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.