Manchester United yaomba radhi

Manchester United imeomba radhi na kujitolea kulipa gharama zozote zilizotokea, kufuatia tafrani iliyozuka katika vyumba vya kubadilishia nguo, kwenye uwanja wa Wembley, katika siku ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA.

Image caption Kulikuwa na mvutano uwanjani

United imesema ilikifahamisha chama cha soka cha England, FA, kuhusiana na ukuta ulioharibiwa kufuatia United kufungwa bao 1-0 na mahasimu wao Manchester City.

United imesema ukuta "haukuharibika sana" na sio meneja Alex Ferguson wala wachezaji walihusika na hilo.

FA imesema haidhani kama itachukua hatua zozote kuhusiana na tukio hilo.