Hatimaye Torres apata goli

Hatimaye Fernando Torres amemaliza ukame wake wa magoli, baada ya kupata bao na Chelsea kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya West Ham.

Image caption Torres hatimaye apata goli akiwa Chelsea

Torres aliingia kama mchezaji wa akiba kipindi cha pili, akiichezea Chelsea kwa mara ya 14, tangu ahamie kutoka Liverpool kwa pauni milioni 50.

Aliachia mkwaju na kuandika bao la pili.

Frank Lampard tayari alikuwa ameipatia Chelsea bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza.

West Ham walipoteza nafasi nyingi, kabla ya Torres kufunga bao la pili, lakini hata Hivyo West Ham ilizamishwa na bao la tatu lililofungwa na Florent Malouda.

Chelsea sasa ina tofauti ya pointi sita nyuma ya Manchester United wanaoongoza ligi ikiwa imesalia michezo minne kumalizika kwa msimu.

West Ham wametitia mkiani.