Manchester United waishinda Everton

Manchester United waishinda Everton na 1-0 na kufungua pengo la pointi 9 dhidi ya wapinzani wake.

Image caption Javier Hernandez

Javier Hernandez alifunga bao kwa kichwa katika dakika za mwisho mwisho kutokana na krosi ya Antonia Valencia .

Alex Ferguson sasa anahitaji pointi saba katika michuano iliyosalia ili kunyakua ubingwa wa Ligi ya Premier.

Manchester United Walijifunga kibwebwe uwanjani Old Trafford lakini katika dakika za mwisho mwisho walionekana kulishambulia mtawalio goli la Everton na ndipo Hernandez akafunga bao.

Manchester United sasa wanaelekea Ujerumani kushiriki katika mechi za nusu fainali dhidi ya Schalke Jumanne katika michuano ya Champions League.