Waandamanaji wameuwawa mjini Aden, Yemen

Watu kama watatu wameuwawa katika mji wa Aden, kusini mwa Yemen, katika mapambano baina ya askari wa usalama na waandamanaji wanaopinga serikali.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Wakuu wanasema wawili kati yao ni askari waliojaribu kuondoa vizuizi vilivowekwa na waandamanaji.

Mmoja alikuwa raia.

Ghasia zimezuka wakati ujumbe wa nchi za Ghuba umewasili Yemen, na mapendekezo yaliyofikiwa katika mazungumzo na Rais Ali Abdullah Saleh, ya kumaliza fujo za kisiasa.

Mapendekezo yanaahidi kuwa Rais Abdullah atapata kinga, ya kutoshtakiwa, ikiwa atajiuzulu.