Kenya na Ufalme wa Uingereza

Nchini Kenya mwaka wa 1952, utasalia kwenye kumbukumbu zake daima.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mfalme George wa IV

Elizabeth Windsor alienda kulala akiwa mwana mfalme na kuamka asubuhi akiwa malkia Elizabeth. Hii ni kufuatia habari za kifo cha baba yake Mfalme George VI.

Miaka 58 baadaye, katika eneo hilo hilo alokuwa kwenye mapumziko yake malkia, katikati mwa Kenya, japo umbali wa takriban kilomita mia moja hivi, mjukuu wake Prince William akamposa mchumba wake Kate Middleton. Na huu umekuwa uhusiano wa kipekee kati ya Kenya na familia ya kifalme ya Uingereza.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Malkia Elizabeth na mumewe Prince Phillip

Nilitembelea chumba alimolala malkia. Chumba hiki kijulikanacho kama Princess Elizabeth Suite kiko katika hoteli ya Treetops, karibu sana na Mlima Kenya. Chumba chenyewe kina ukubwa wa futi saba kwa nane, kuna kitanda kikubwa na kwenye ukuta mmoja kuna picha ya malkia Elizabeth, Mumewe na marehemu mamake, Princess Diana.

Image caption Prince Charles na Lady Diana

Chumba hiki kina taswira tofauti na vyumba vingine kwenye hoteli hii ambapo Princess Elizabeth Suite ina bafu na choo yake kando.

Chumba hiki kipo kwenye ghorofa ya pili na upande mmoja kuna mlango wa kioo ambao unaelekeza ubaraza wa ghorofani. Hapa mgeni anaweza kuwaona wanyama wa pori wanaokuja kunywa maji katika dimbwi lililopo katika eneo la hoteli hiyo.

Haki miliki ya picha PHIL NOBLEAFPGetty Images
Image caption William na Kate

Ingawa waliokuwa wakifanya kazi katika hoteli hii wakati huo wengi wameaga dunia, niliongea na Stephen Kabatha, ambaye ni mtaalam na msimamizi wa wanyama na mimea katika hoteli hii. Amekuwa akifanya kazi hapa kwa muda wa miaka tisa sasa.

"Chumba hiki ni tofauti kidogo na kile alimolala mwaka wa 1952 maanake chumba hicho kiliungua mwaka 1954 na wapiganaji wa MauMau waliokuwa wakipigania uhuru wa Kenya kutoka kwa mkoloni," Stephen alinieleza .

Chumba kipya kilijengwa mwaka wa 1957. Malkia Elizabeth alirudi katika hoteli ya Treetops mwaka wa 1983.

Haki miliki ya picha
Image caption Kate na William

"Alifurahi alipoona kwamba choo na bafu zimejengwa pamoja katika chumba hiki. Lakini kile alichoona tofauti ni kwamba alipokuwa hapa zamani kulikuwa na misitu mingi lakini wakati aliporudi alipata idadi ya wanyama imeongezeka zaidi na wanyama wameharibu misitu," Stephen alisema.

Lakini si hoteli ya Treetops peke yake ambayo inaonekana kuvutia familia ya kifalme ya Uingereza. Takriban kilomita 100 kutoka Treetops, katika uwanda wa Lewa, kuna sehemu juu ya mlima Kenya ijulikanayo kama Rutundu. Ni hapa mwaka wa 2010 ambapo mjukuu wa malkia Elizabeth, Prince William alimposa mchumba wake Kate Middleton.

Stephen anasema matukio haya yameinua sifa ya Kenya na kuwavutia wageni maarufu ikiwa ni pamoja na marais kutoka nchi za Urusi, Zambia na Tanzania.