Man City yaishinda Blackburn Rovers

Dzeko Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Edin Dzeko

Goli la kwanza la Edin Dzeko katika ligi kuu ya England limeongeza matumaini ya Manchester City kucheza ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kuifunga Blackburn Rover inayochechemea.

City walianza kwa kasi, huku mkwaju wa David Silva ukigonga mwamba.

Chris Samba wa Rovers alijibu kwa kuruka kichwa, huku Jason Roberts akichelewa kuufuata mpira.

Lakini dakika tatu baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba katika kipindi cha pili, Dzeko alivurumisha shuti na kumpita kipa Paul Robinson.

Hili ndio goli la kwanza la Dzeko katika michezo tisa ya ligi kuu.

City sasa ina pointi 59, pointi tano nyuma ya Arsenal, huku Blackburn ikichungulia shimo ikiwa na pointi 35.