Watu waandamana dhidi ya ziara ya Mfalme Mswati

Mfalme Mswati
Image caption Mfalme Mswati

Ikiwa imesalia siku mbili tu kabla harusi ya mwana mfalme William na mchumba wake Kate Middleton, mamia ya raia wa Swaziland na wanaharakati a kutetea haki sawa, wamefanya maandamano mjini London.

Watu hao wanapinga ujio wa Mfalme Mswati wa Swaziland ambaye amealikiwa kuhudhuria harusi hio.

Wanasema safari yake itagharimu nchi hiyo maskini, fedha nyingi ambazo bora zitumiwe kufadhili huduma za afya na maji nchini Swaziland.