Besigye ametoka hospitali Nairobi

Siku moja baada ya kutoka hospitali mjini Nairobi, kiongozi wa upinzani nchini Uganda anasema anajiandaa kurudi nyumbani.

Haki miliki ya picha AFP

Dr. Besigye anasema ataporudi huko ataendelea na harakati zake, za kutembea hadi kazini.

Kwa sasa anasema afya yake imetengenea kiasi na anaweza kuona, japo macho bado yanamsumbua.

Alikuwa akizungumza mjini Nairobi alipokuwa anapata matibabu.

Alisema "bila ya shaka nitarudi Uganda, sina nchi nyengine, ni nchi yangu na ni lazima nirudi Uganda.

Vitendo tunavoshughulika navyo hivi sasa, siyo vitendo vyangu, ni vitendo vya wananchi wa Uganda, ambao wameamua lazima wajirudishie uwezo na kuona kwamba mali ya umma inawahudumia, siyo inawahudumia wale wachache. Na wakati wanapigania haki zao, sisi wote viongozi tutaendelea kuwaunga mkono, na kufanya chochote ambacho kitasaidia kuleta mabadiliko yanayohitajika nchini mwetu."