Wazee maarufu wanazuru Ivory Coast

Ujumbe wa Wazee Maarufu unazuru Ivory Coast, kujaribu kuhimiza umoja na mapatano baada ya ghasia zilizofuatia uchaguzi, ambapo watu mamia kadha waliuwawa.

Haki miliki ya picha AP

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, anayeongoza ujumbe huo, alisema hali nchini humo bado ni tete.

Ghasia za hapa na pale zimeendelea, tangu rais wa zamani, Laurent Gbagbo, kukamatwa mwezi uliopita; na Bwana Alassane Ouattara kuchukua uongozi.

Wengine kwenye ujumbe huo wa wazee, ni Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini na rais wa zamani wa Jamhuri ya Ireland, Mary Robinson.