Norwich yapanda daraja

Norwich City imerejea tena katika ligi kuu ya England baada ya kumaliza katika nafasi ya pili katika ligi daraja la kwanza nyuma ya QPR.

Norwich imefuzu baada ya kupata ushindi dhidi ya Portsmouth na pia kufuatia Cardiff kufungwa na Middlesbrough.

Mara ya mwisho Norwich kucheza ligi kuu ilikuwa miaka sita iliyopita.