Man United kucheza fainali na Barcelona

Manchester United itakutana na Barcelona kwenye fainali ya klabu Bingwa Ulaya baada ya kuichapa Schalke 04 ya Ujerumani kwa magoli 4-1.

Image caption Man United

Magoli ya Manchester United yalifungwa na Antonio Valencia, Darron Gibson, na Anderson kufunga magoli mawili.

Katika mchezo wa kwanza Man United ilipata ushindi wa mabao 2-0.

Barcelona iliingia fainali baada ya kuifunga Real Madrid 3-1 baada ya michezo miwili ya nusu fainali.

Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya itachezwa kwenye uwanja wa Wembley, tarehe 28 mwezi Mei.