DR Congo: 48 Wanabakwa kila saa

Muadhiriwa wa ubakaji nchini Congo
Image caption Muadhiriwa wa ubakaji nchini Congo

Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Marekani umeonyesha kuwa takriban wanawake na wasichana 48 wanabakwa kila saa katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida moja la afya,umegundua kuwa wanawake 400,000 kati ya umri wa miaka 15-49 walibakwa katika muda wa miezi 12 kati ya mwaka 2006 na 2007.

Idadi hii ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya awali ya kuonyesha kuwa wanawake 16,000 wanabakwa katika muda wa mwaka mmoja iliyotangazwa na umoja wa mataifa.

Serikali ya DRC inasema hali hii ya sasa inaonyesha kuwa wanawake wana nafasi ya kutoa taarifa zaidi juu ya matukio ya ubakaji.

Ubakaji umekuwa kama jambo la kawaida katika mapigano yanayoendelea mashariki mwa Congo.

Amber Peterman, mtafiti mkuu,anasema: "utafiti wetu umedhihirisha kuwa idadi ya matukio ya awali haionyeshi hali halisi ya matukio ya ubakaji yanayoendelea kujitokeza nchini Congo.