Dawa 'inapunguza' maambukizi ya HIV

Watoto wakihimiza, uhumimu wa kuzuia maambukizi wa ukimwi Haki miliki ya picha XINHUA
Image caption Watoto wakihimiza, uhumimu wa kuzuia maambukizi wa ukimwi

Mtu anayeishi na virusi vya HIV na anayetumia dawa za kupunguza makali punde tu anapogundua,kuliko wakati ambao afya yake imezorota kabisa,anaweza kupunguza kumuambukiza mtu ambaye hana virusi hivyo kwa asilimia 96%, haya ni kwa mujibu wa utafiti.

Taasisi ya kitaifa ya afya ya Marekani ilifanya utafiti huo kwa wapenzi 1,763 huku katika kila kundi la wapenzi kukiwa na mmoja anayeishi na virusi vya HIV.

Kutokana na mafanikio yake makubwa,utafiti huo ulisitishwa miaka minne kabla ya muda wake uliopnagwa.

Shirika la afya duniani WHO linasema utafiti huu ni "mafaniko muhimu".

Utafiti ulianza mwaka 2005 katika vituo 13 barani Afrika, Asia na Marekani.

Wanaoishi na virusi vya HIV waliwekwa katika makundi mawili.Katika kundi moja,watu walipewa dawa za kupunguza makali ya HIV mara moja.

Kundi lengine wakapewa dawa hizo baada ya muda kidogo.

Makundi yote mawili walipewa ushauri ya kutumia mbinu salama wakati wa kujaamiana,mipira ya kondomu bila malipo na kutibiwa magonjwa yanayopatikana kwa kujaamiana.

Miongoni mwa wale ambao walianza kutumia dawa hizo mapema kulikuwa na tukio moja tu la wapenzi kuambukizana.

Katika kundi lengine kulikuwa na matukio 27 ya maambukizi.