Ajali nyingine ya boti DRC

Mitumbwi nchini DRC

Zaidi ya watu 100 wanahofiwa kufa baada ya chombo walimokuwa ndani kuzama katika Ziwa Kivu, kusini mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mwandishi wa BBC, amesema ajali hiyo ilitokea katika mji wa Tshikapa, Kusini mwa DRC. Ajali hiyo ilitokea jumapili usiku.

Mashua hiyo ya kusafirisha mizingo inasemekana ilizama ikiwa na zaidi ya watu 300.

Maafisa wanasema idadi kamali ya watu waliofariki haijulikana. Hata hivyo watu 30 wanasemekama wamenusurika baada ya kuogelea hadi kwa ufukwe wa ziwa hilo.

Ajali ya sasa imetokea wiki moja baada ya watu 50 kufa katika ziwa hilo upande wa Mashariki, pale mtumbwi wao ulipozama. Shughuli za uokozi zinaendelea.