Tunisia: Mashtaka zaidi kwa Ben Ali

Aliyekuwa kiongozi wa Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali na mkewe wanatarajiwa kukabiliana ma mashtaka mapya yanayohusishwa na mauaji ya baadhi ya waandamanaji wakati wa ghasia za mwezi Januari.

Bw Ben Ali aliondolewa madarakani baada ya wiki kadhaa za maandamano na kukimbilia Saudi Arabia.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Tunisia

Tayari anakabiliwa na mashtaka 18 tofauti , ikiwemo kuua kwa kukusudia na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Waziri wa sheria alisema, mashtaka haya mapya ni pamoja na "kuchochea ghasia, mauaji na uporaji" na "kufanya njama dhidi ya usalama wa ndani."

Kulingana na shirika rasmi la habari Tap, mashtaka hayo mapya yanafanyiwa uchunguzi na mahakama kwenye mji wa Sousse ulio pwani ya nchi hiyo.

Chanzo kutoka wizara ya sheria kimeiambia shirika hilo la habari, yameanza kwenye tukio lililotokea katikati ya mji wa Ouardanin jioni ya Januari 15 hadi asubuhi ya Januari 16.

Majeshi ya usalama yaliua watu wanne baada ya kuwafyatuliya risasi waandamanaji waliokuwa wakijaribu kumzuia mpwa wa Bw Ben Ali, Kais Ben Ali, kukimbia mji huo.

Bw Ben Ali na mkewe Leila Trabelsi walikimbilia Saudi Arabia Januari 14.

Haki miliki ya picha
Image caption Mke wa Bw Ben Ali

Maafisa wa usalama 14 wameshtakiwa kutokana na kuhusishwa na ufyatuliaji risasi Ouardanin.

Aliyekuwa rais wa nchi hiyo anashtumiwa kuamuru majeshi hayo kufyatua risasi.

Umoja wa mataifa unasema watu 210 waliuawa wakati wa ghasia za Tunisa zilizoanza katikati ya Desemba.