Mourinho apewa adhabu

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amepewa adhabu ya mechi tano kwa mechi za Ulaya, kutokana na matukio wakati wa nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya, dhidi ya Barcelona.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jose Mourinho

Chama cha soka Ulaya, UEFA, kimesema Mourinho alitoa matamshi "yasiyofaa", baada ya Real Madrid kufungwa 2-0 na Barcelona, akiwatuhumu waamuzi kwa kujaribu kuisaidia Barcelona.

Mourinho tayari ametumikia adhabu ya mchezo mmoja kukaa jukwaani, katika mchezo wa pili, na michezo mingine mitano itatekelezwa iwapo atafanya makosa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

UEFA pia imemfungia kutocheza mchezo wa fainali kipa wa Barca wa akiba Jose Pinto.