Taliban inashambulia vikali Kandahar

Shughuli zimesimama katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Afghanistan, mji wa Kandahar, kusini mwa nchi, kwa sababu ya mapigano makali, yaliyozushwa na mashambulio kadha yanayofikiriwa kufanywa na wapiganaji wa Taliban dhidi ya majengo ya serikali.

Haki miliki ya picha ap

Mashambulio kama sita yamefanywa na watu waliojitolea mhanga.

Mapigano mengi yametokea kwenye maeneo ya biashara.

Watu wengi walijeruhiwa.

Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, alisema Taliban wanajaribu kuficha kuwa wameshindwa kwa Osama Bin Laden kuuwawa, kwa kulipiza kisasi kwa kushambulia raia wasiokuwa na hatia.

Taliban imekanusha kuwa mashambulio hayo ni ya kujibu mauaji ya Bin Laden, na wamesema mashambulio hayo yalipangwa kitambo.