Ubingwa wanukia Man United

Manchester United inahitaji pointi moja kutangazwa bingwa wa ligi kuu ya England, baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya Chelsea kwa mabao 2-1.

Image caption Man U ikicheza na Chelsea

Magoli ya Havier Hernandez katika dakika ya kwanza na bao la kichwa la Nemanja Vidic yaliipa ushindi muhimu kwa Manchester United kusogelea ubingwa.

Goli pekee la Chelsea lilifungwa na Frank Lampard.

United walitawala zaidi kipindi cha kwanza, huku Chelsea wakipigana kufa na kupona katika kipindi cha pili.

Man United itakutana na Blackburn Jumamosi ijayo.

Arsenal yafungwa

Haki miliki ya picha Other
Image caption Mashabiki wa Stoke

Katika michezo mingine Arsenal imefungwa mabao 3-1 na Stoke City na kuthibitisha Arsenal kumaliza msimu bila ya kombe lolote.

Baada ya kuichapa Man U, Arsenal walikuwa na ari kubwa ya kushinda mechi zote zilizosalia, lakini walishindwa kutamba mbele ya Stoke.

Kenwyne Jones aliandika bao la kwanza la Stoke, huku Jermaine Pennant akipachika la pili na la tatu kufungwa na Jonathan Walters.

Bao pekee la Arsenal lilifungwa na Robin Van Persie.

Huko mkiani katika ligi kuu Wolverhampton imejisogeza hadi nafasi ya 17 baada ya kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya West Brom.