Pakistan wito wa viongozi kujiuzulu

Marekani inasema Osama Bin Laden alikuwa hakujitenga bali akiongoza Al Qaeda hadi alipouliwa na kikosi cha Marekani nchini Pakistan juma lilopita.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Osama BIn Laden

Na nchini Pakistan viongozi wa serikali na jeshi wamekuwa na kikao cha dharura huku kuna wito kuwa Waziri Mkuu na Rais wanafaa kujiuzulu.

Rais wa Pakistan, Waziri Mkuu na mkuu wa jeshi wamekuwa na kikao hicho baada ya kuuwawa kwa Osama Bin Laden.

Inaelekea wana hamu ya kutafuta njia ya kuokoa jahazi kuna ripoti kuwa taarifa rasmi itatolewa kesho bunge likikutana.

Swala muhimu ni nani alikuwa akijua kuwa bin Laden alikuwa ndani ya nchi na kama wanasiasa waliambiwa.

Nguvu ziko mikononi mwa jeshi nchini Pakistan.

Na kama jeshi llikuwa linajua kuwa Bin Laden akiishi nchini na likaificha serikali basi itaonesha kuwa serikali haina mamlaka juu ya nchi.

Tangu hapo serikali ilikuwa imeshadhoofika kutokana na shida za kiuchumi lawama wakati wa mafuriko makubwa ya mwaka jana na uhusiano wake na Marekani, huku ndege za Marekani zisokuwa na rubani zinaendelea kufanya mashambulio katika ardhi ya Pakistan.