Mutharika: balozi wa Ungereza alinitusi

Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika, ameeleza sababu ya kumfukuza balozi wa Uingereza mwezi uliopita.

Haki miliki ya picha PA

Katika taarifa yake ya mwanzo kuhusu ugomvi huo, Rais Mutharika alisema Balozi Fergus Cochrane-Dyet alimtusi, na hayuko tayari kukubali hayo, eti kwa sababu Malawi inapata msaada wake mkubwa kabisa kutoka Ukngereza, kushinda nchi nyengine.

Magazeti yalichapisha barua iliyofichuliwa, ambamo Balozi Cochrane-Dyet alimuelezea Rais Mutharika kuwa anaongoza kimabavu, na hakubali kukosolewa.

Uingereza ilimtaka balozi wa Malawi aondoke London, kujibu kufukuzwa kwa Bwana Cochrane-Dyet kutoka Malawi.