Barcelona mabingwa La Liga

Barcelona wamechukua ubingwa kwa mara nyingine tena wa ligi kuu ya Uhispania baada ya kutoka sare na Levante na kupata pointi moja iliyosalia kutangazwa washindi.

Haki miliki ya picha Other
Image caption Messi wa Barca

Barca wamechukua ushindi huu kwa mara ya tatu mfululizo, baada ya kufikisha pointi 92 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine msimu huu.

Mahasimu wao Real Madrid wamechukua nafasi ya pili.