Kampala ulinzi mkali

Kizza Besigye.
Image caption Kizza Besigye.

Serikali ya Uganda imeimarisha usalama katika mji mkuu Kampala,huku kiongozi wa upinzani akitarajiwa nchini Jumatano asubuhi.

Kizza Besigye,anatokea mjini Nairobi ambako amekuwa akipokea matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata wiki mbili zilizopita.

Serikali ya Uganda nayo inajiandaa kuwakaribisha viongozi wa nchi mbali mbali kwa sherehe ya kuapishwa ya rais Yoweri Museveni siku ya Alhamisi.

Rais Museveni ameonya wale wanaotaka kuvuruga shughuli hiyo yake kwamba watakabiliwa na sheria,rais alisema hayo akiwa nyumbani kwake magharibi mwa Uganda alipohutubia mkutano wa waandishi wa habari.

Image caption Yoweri Museveni

Museveni amesema kwa vyovyote vile hafla hiyo itaendelea, '' Nimeskia watu wengine,wanataka kusimamisha shughuli yangu,hakuna mtu atazuia hiyo shughuli labda Mungu peke yake,'' Alisema Museveni.

Aliongeza kusema kwamba kama viongozi lazima waheshimu serikali iliyochaguliwa kwa njia ya demokrasia ingawa alikiri kuwa polisi walipita mipaka wakati walipokuwa wanamkamata Kizza Besigye.