Ferguson ashtakiwa kwa kumsema mwamuzi

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameshtakiwa na chama cha soka cha England,FA, kufuatia matamshi aliyotoa kuhusu mwamuzi Howard Webb.

Image caption Sir Alex Ferguson

Alitoa matamshi hayo kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Chelsea ambapo United walipata ushindi wa mabao 2-1.

Licha ya kuwa Ferguso hakumsema vibaya Webb, lakini alivunja sheria ya FA, ambayo inasema hakuna meneja anaruhusiwa kuzungumzia mwamuzi kabla ya mchezo.

Ferguson amepewa hadi Mey 16 kuwasilisha utetezi wake.

Manchester United aliichapa Chelsea 2-1 Jumapili iliyopita na kubakiza pointi moja kupata ubngwa wa ligi kuu, huku ikiwa imesalia michezo miwili.

Lakini siku mbili kabla ya mchezo huo - ambao Chelsea wangeshinda wangekwenda kileleni katika msimamo - Ferguson alimzungumzia Webb katika mkutano na waandishi wa habari.