TP Mazembe yatolewa, Simba kusonga mbele

Mabingwa watetetezi wa Klabu Bingwa Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imeondolewa katika michuano ya klabu bingwa Afrika.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption TP Mazembe

Shirikisho la Soka barani Afrika Caf limechukua hatua hiyo kufatia malalamiko ya Simba ya Tanzania kuhusu kuchezeshwa kwa Janvier Besala Bokungu.

Mazembe iliichapa Simba 6-3 katika mechi mbili walizocheza.

Simba sasa itapambana na Wydad Casablanca ya Morocco, ambayo ilifungwa na Mazembe katika raundi ya tatu, kupata nafasi ya katika ngazi ya makundi.

Simba na Wydad casablanca watakutana katika uwanja utakaotangazwa wiki ijayo.

Mazembe imeshinda ligi ya mabingwa Afrika kwa miaka miwili iliyopita, na kufika fainali ya klabu bingwa ya Dunia mwaka jana, na kutolewa na Inter Milan ya Italia kwa mabao 3-0.