Sudan Kaskazini inashinda Kordofan

Serikali ya Sudan imeshinda katika uchaguzi wa gavana katika jimbo muhimu, kwenye uchaguzi ambao ulianiwa vikali na chama kinachotawala Sudan Kusini.

Haki miliki ya picha AFP

Jimbo la Kordofan Kusini lina mafuta mengi ya Sudan Kaskazini, lakini piya lina watu wengi wa kabila la Wanubi, ambao wengi walipigana pamoja na Sudan Kusini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivomalizika mwaka wa 2005.

Gavana aliyechaguliwa, Ahmed Haroun, anasakwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, kwa tuhuma za uhalifu wakati wa vita.

Sudan Kusini inatarajiwa kupata uhuru kutoka Sudan Kaskazini, mwezi wa July.