Ebola imeuwa mtu Uganda

Msichana wa miaka 12 amekufa nchini Uganda kutokana na virusi vya Ebola, kwenye mji kaskazini ya Kampala.

Afisa wa serikali anayehusika na afya ya jamii, Dr Anthony Mbonye, alisema ukaguzi uliofanywa kwenye maabara umethibitisha kuwa msichana huyo akiugua Ebola, na kwamba anahofia watu wengine wataambukizwa ugonjwa huo, na wao wanajitahidi kuudhibiti:

Dr Mbonye alitoa ushauri huu kwa watu wa Uganda ili kujikinga na ugonjwa huo unaouwa:

"Wanaogusa maiti ya watu waliokufa kutokana na Ebola, lazima wajikinge kwa kuvaa vitu vya kuwahifadhi, na maiti wazikwe haraka, na kusifanywe karamu na mkusanyiko mazikoni.

Na tunawaomba watu wasile nyama ya mzoga hasa nyama ya tumbile.

Wizara ya afya inawaomba watu kuwa watulivu kama inavowezekana, kwa sababu hatua tulizochukua zitadhibiti ugonjwa huo."