Msaada wa chakula ni haba Somalia

Shirika la Chakula Duniani, WFP, linasema linabidi kupunguza posho inazogawa nchini Somalia, na inawaacha maelfu bila ya chakula kwa sababu halina fedha za kutosha.

Shirika hilo linasema akiba ya chakula ni thuluthi tu ya kile kinachohitajika kuwalisha Wasomali milioni moja wanaohitaji msaada kwa sababu ya ukame na vita vya mika mingi.

WFP inasema inahitaji dola milioni 53, kugharimia mahitaji ya Somalia hadi mwisho wa mwaka, na itakutana na wafadhili katika wiki chache zijazo.