Ashton kufungua ubalozi Libya

Mkuu wa Idara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton, anazuru eneo la Libya linalodhibitiwa na wapiganaji, kufungua ubalozi mjini Benghazi, mashariki mwa nchi.

Image caption Bi Ashton

Bi Ashton alisema hiyo ni ishara kuwa Umoja wa Ulaya unaunga mkono watu wa Libya.

Kabla ya Catherine Ashton kuwasili Benghazi, ndege za NATO zilifanya shambulio jengine dhidi ya maeneo ya serikali mjini Tripoli, pamoja na eneo la nyumba ya Kanali Gaddafi.

Katika mkutano Bi Ashton alizungumuzia ufadhili katika kudhibiti mipaka, mageuzi ya miundombinu ya usalama, na mahitaji ya kuimarisha uchumi, afya na elimu pamoja na maslahi ya raia wa nchi hiyo.