Marekani hatimaye itazungumza na Taliban

Alipohojiwa na BBC, kabla ya kuanza ziara yake Uingereza Jumatatu, Rais Obama ameonesha kuwa atakuwa tayari kuamrisha operesheni nchini Pakistan, dhidi ya kiongozi mwengine wa Al Qaeda au Taliban.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Ingawa Rais Obama alisema yuko tayari kuchukua hatua dhidi ya Mullar Omar kiongozi wa Taliban, lakini kauli yake ilikuwa tafauti kuhusu vita dhidi ya Taliban nchini Afghanistan.

Alifahamisha wazi kuwa vita virefu kabisa vya Marekani vinaweza kumalizika kwa mazungumzo na adui:

"Hatuwezi kumaliza tatizo hili kwa vita.

Tunachoweza kufanya ni kutumia mafanikio tuliyopata kijeshi kutafuta suluhisho la kisiasa.

Inamaanisha kuwa hatimaye lazima tuzungumze na Taliban, ingawa tumeweka shuruti kabla ya mazungumzo ya maana kufanyika.

Taliban lazima ikate uhusiano na Al Qaeda, iache kutumia nguvu, na itabidi iheshimu katiba ya Afghanistan."