Jina lililofichwa laanikwa hadharani

Hatimaye jina la mcheza soka ambaye lilizuiwa na mahakama kutajwa na vyombo vya habari nchini Uingereza, sasa limetajwa hadharani.

Image caption Ryan Giggs

Mchezaji huyo ambaye ameoa na kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa ametajwa kuwa ni Ryan Giggs wa Manchester United.

Jina hilo lilitajwa na mbunge John Hemming kupitia kifungu cha bunge kinachoruhusu kuvunja amri ya mahakama.