Unamfahamu Oprah Winfrey?

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Oprah Winfrey, Rais Obama na mkewe Michelle

Moja ya vipindi vinavyotazamwa sana katika historia ya Marekani, The Oprah Winfrey Show, kinamalizika baada ya miaka 25. Kipindi chake kimegusa wengi na kuvuka mipaka ya televisheni.

Kipindi chake cha kwanza, kilichoitwa Namna ya Kumwoa au Kuolewa na mtu wa Chaguo lako, kilipendekezwa kiwe kipindi kinachorushwa mchana kama kipindi chengine chochote cha kawaida.

Lakini baada ya vipindi 4,560, watu maarufu kama Madonna, Beyonce na Tom Hanks wanatarajiwa kutokea kwenye kipindi chake cha mwisho cha kuagwa, kinachorushwa hewani siku ya Jumatano.

Wakati wa miaka hiyo 25, Winfrey limekuwa jina maarufu sana, anayekubalika na wengi na ni mmoja wa matajiri katika ulimwengu huu.

Akimaliza na kuendelea kufanya kazi katika televisheni yake mwenyewe, uwezo wa kupata wageni wanaovutia kwenye habari haliwezi kudharauliwa.

Mwezi huu, Rais Obama alizungumzia kwanini alihitaji kutoa cheti chake cha kuzaliwa hadharani.

Na Sarah Ferguson alizungumzia kwanini hakualikwa kwenye harusi ya kifalme Uingereza.

Kwahiyo ni namna gani ambavyo Winfrey ameweza kufanikiwa? Mambo 10 yanajumuisha ushawishi wake.

ATOA MADAI YA KUDHALILISHWA KIJINSIA, 1986

Image caption Oprah Winfrey

Katika hatua yake ya kukiri ambapo baadae ikaja kuwa namna ambavyo anafanya kazi, Oprah aliwaambia watazamaji wake kuwa alibakwa alivyokuwa mtoto.

Si kwamba tu ilisababisha mwanzo wa kampeni isiyo rasmi kuhusu udhalilishaji, iliweka njia kwa msururu wa watu-maarufu wenye mtawaliwa, watu wa kawaida wenye mambo ya kueleza- kukaa kwenye kochi lake na kukiri.

Mwandishi wa vitabu Bonnie Greer, aliyeondoka kwao Chicago mwaka huo huo ambao Oprah alianza kupanda chati mjini humo, alisema: " Amefanya mawazo yaliyo ya wengi yakubalike kirahisi lakini anaielezea kama inamhusu moja kwa moja mwanamke wa Kimarekani mweusi.

"Imekuwepo siku nyingi katika utamaduni wa Kimarekani, lakini Oprah aliileta kwenye televisheni wakati wa mchana. Alianzisha utamaduni wa "mwathirika" kwa mantiki ya uzuri na ubaya.

"Aliingia wakati wa msukosuko wa uchumi katikam iaka ya mwisho ya 80 na mwanzo wa 90, jambo ambalo Wamarekani walitaka kuhakikishiwa: namna ya kuhimili na uzuri wetu.

"Oprah alizungumzia vitu kwa waliokuwa wakitazama vipindi vyake kwasababu alitaka kuonyesha 'uzuri' na 'uaminifu' yana malipo yake hapa duniani.

MKOKOTENI WA MAFUTA, 1988

Akiwa amevaa jeans ya saizi 10, Winfrey aliyekuwa mwembamba aliingia kwenye jukwaa wakati wa kipindi chake na mkokoteni wa mafuta kuonyesha namna alivyopoteza kilo 30 kwa kipindi cha miezi minne kwa kutokula kitu zaidi ya Optifast.

Lakini uzito ukaanza kurudi na ikawa mwanzo wa miongo miwili ya kupunguza kiwango cha kula na kupambana ili kukifanya kiuno kiwe kidogo.

Tim Teeman, mwandishi wa Marekani wa gazeti la Times, alisema: " Ikiwa Oprah atakumbukwa kwa lolote, basi ni umbo lake."

"Unaweza kusema haitoi ujumbe wa kweli lakini unatoa ujumbe sahihi. Jinsi Oprah alivyozungumzia uzito ni hali halisi ya namna watu mbalimbali wanavyopambana na uzito wao.

MICHAEL JACKSON ATOBOA, 1993

Idadi kubwa ya waliokuwa wakiangalia kipindi cha Winfrey illiongezeka alipomhoji Michael Jackson wakati umaarufu wake ulipozidi kupamba moto.

Takriban watazamaji milioni 62 walimwona ndani ya Neverland mtu aliyenaswa kwenye utoto wake, kabla ya madai ya kudhalilisha watoto kuibuka na kumharibia sifa yake.

Wakati wa mahojiano yaliyochukua dakika 90, alimwambia alikuwa akiumwa maradhi ya ngozi na alikana kuwa alilala kwenye chumba chenye gesi ya oksijeni.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Michael kuzungumza kwa muda mrefu katika kipindi cha miaka mingi na ilionekana kuwa jambo la kipekee kwa kipindi cha Winfrey, na kuandikwa kwenye vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali duniani na kusaidia kuimarisha sifa yake.

ELEN DEGENERES AJITOA HADHARANI, 1997

Mchekeshaji wa Marekani, mwendesha kipindi kwenye televisheni na muigizaji Ellen DeGeneres alisema hadharani kuwa anafuata mapenzi ya jinsia moja kwenye kipindi hicho.

Mahojiano hayo yalifungua mlango upya kwa kazi ya DeGeneres ambaye alianzisha kipindi chake mwenyewe cha mahojiano.

Mvuto wa Winfrey kwa wanawake wengine umejadiliwa sana.

Greer alisema, " Ni mtetezi wa wanawake kwa minajil ya kwamba amejenga milki yake mwenyewe na mfano wake umesababisha wanawake wengine kuiga."

"Ni wazi kwa hakika anakupa msukumo, hodari sana na mwerevu na amefanya mambo mazuri. Kila mmoja anamtakia kheri, pamoja na mimi.

Licha ya kukiri kuhusu masuala yake ya uzito na udhalilishaji, na uwezo wake wa kufanya wengine kama DeGeneres kuwa wazi, inashangaza namna ambavyo tunajua machache kuhusu Winfrey mwenyewe, alisema Greer.

" Kila mmoja aliye karibu yake hazungumzii mambo yake. Ni miongoni mwa watu maarufu Marekani ambao tunajua kila kitu na hatujui kitu vile vile.

TOM CRUISE JUU YA KOCHI, 2005

Huenda wakati utakaokumbukwa zaidi kwa Oprah ni pale Tom Cruise alipoanza kuchekacheka, akiruka juu na chini kwenye kochi lake alipoelezea penzi lake kwa mpenzi wake mpya, Katie Holmes, ambaye kwa sasa ni mke wake.

Teeman alisema tangu wakati huo tendo lake hilo limekuwa likifanyiwa dhihaka na kuigwa kwa kubezwa. Huu ni wakati ulioainisha kazi yake, baada ya filamu kama Top Gun, Cocktail au Mission Impossible.

"Oprah alionekana kumahanika, akifikiria 'Anafanya nini?' Kazi yake iliporomoka kwa muda lakini amerudi."

Watu maarufu hushiriki kipindi cha Oprah kuondosha pepo mbaya au kukiri jambo la kimapenzi, alisema, na wanajua hatowapa wakati mgumu.

JAMES FREY ALAANIWA, 2006

Moja ya ushawishi mkubwa aliokuwa nao Winfrey umekuwa katika ulimwengu wa uchapishaji vitabu, klabu yake ya vitabu imekuwa kisifiwa kwa kutengeneza mamilioni kwa waandishi ambao vitabu vyao hujadiliwa kwenye klabu yake.

Hakuna pahala ambapo ushawishi wake ulionekana kama katika kesi ya James Frey. Kitabu chake cha A Million Little Pieces, iliyoelezea hadithi yake ya kujikwamua kutokana na matumizi ya dawa za kulevya, ambapo ilikuwa kitabu kilichouzwa kwa kiwango kikubwa baada ya kutokea kwenye kipindi chake.

Lakini mwaka 2006, baada ya kuwa na shaka na maisha yake aliyoyaeleza Frey, Winfrey alimwalika tena mwandishi huyo ili kumhoji, iliyosababisha mabishano makali na kuvua nguo hadharani kwa Frey.

Licha ya Winfrey kuelezea hivi karibuni kujuta kwa namna alivyolishughulikia suala hilo, alichojifunza si kukereka, alisema Teeman.

Kipindi chake ni kuhusu nia njema, na kitendo cha kusaliti uaminifu huo ni kuaibika.

SHULE YA AFRIKA KUSINI YAFUNGULIWA, 2007

Image caption Oprah na wanafunzi Afrika Kusini

Shule ya uongozi ya Winfrey, karibu na Johannesburg, ilifunguliwa mwaka 2007 kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 40.

Aliahidi kujenga shule hiyo baada ya kukutana na aliyekuwa rais wa Afrika kusini Nelson Mandela mwaka 2002.

Winfrey mwenyewe aliwahoji wasichana wengi wa Afrika kusini waliotoka kwenye familia maskini walioomba nafasi 150 za mwanzo katika shule hiyo.

Mwaka jana, aliyekuwa matroni wa chuo hicho alifutiwa mashtaka ya kudhalilisha mabinti chuoni hapo.

Winfrey alieleza namna alivyosikitishwa wakati hukumu ilipotolewa lakini alisema anajivunia kwa namna wasichana hao walivyopata ujasiri wa kutoa ushahidi.

Ufadhili wake unajulikana, na wakfu wake wa Oprah Winfrey umechangia mamilioni ya dola kwa miradi Marekani na nchi za nje, huku shirika lake la ihsani Oprah's Angel limechanga kiasi cha dola za kimarekani milioni 80.

BARACK OBAMA, SI CLINTON, 2007

Katika mkutano Iowa mwaka 2007, Oprah Winfrey alimwuunga mkono Barack Obama ambaye kwa wakati huo alikuwa akigombea nafasi ya urais kupitia chama cha Democrat na Hillary Clinton.

Kuunga mkono kwake Winfrey kulionekana kuwa muhimu sana katika mpambano wa karibu wa nafasi hiyo kutokana na ushawishi mkubwa alionayo. Lakini chaguo lake liliacha maswali mengi.

" Alipomwuunga mkono Obama kwa nafasi ya urais watazamaji wake, ambao ni wanawake wazungu wa makamo, walikuwa wakimwuunga mkono Hillary Clinton na akakuta wengi wakimwacha mkono kwa kudhani anachagua asili au jamii yake kuliko jinsia yake. Alisema Eric Deggans, mkosoaji kupitia televisheni ya Petersburg Times huko Florida.

Umaarufu wake mkubwa ulitikisika kwenye jamii ya watu weusi alipokosoa muziki wa miondoko ya rap kwa mashairi yaliyo na chuki kwa wanawake.

Mara zote amekuwa akijiwakilisha kama mweusi lakini si kiais hicho cha kuwapoteza watazamaji walio wengi, alisema Deggens.

Lakini Winfrey ameonyesha, kama alivyofanya Bill Cosby kabla yake na Barack Obama baadae, kinachowezekana kwa Mmarekani mweusi.

"Kwa kufikia kiwango hicho kwenye televisheni, Oprah ameonyesha unaweza ukang'ara kama mtu mweusi.

"Amekuwa sauti ya wanawake weupe wa makamo kwa namna ambavyo haijawahi kufanywa na mtu yeyote, na kwa watu weusi kuona Mmarekani mweusi anakubalika kwa moyo mmoja ni muhimu sana."

KUAGWA NA WATU MAARUFU, 2011

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Tom Hanks akimuaga Oprah

Moja ya vipindi vya mwisho vya Oprah Winfrey huko Chicago uligeuka kuwa usiku uliojaa machozi, shukrani na watu mashuhuri kama vile Tom Cruise, Will Smith na Madonna.

" Jambo kuhusu Oprah ambalo linapendeza ni kwamba ameweza kuunda alama inayojumuisha utata mkubwa.

" Ni rafiki yako halisi ambao marafiki zake ni Julia Roberts na Tom Cruise. Ni kiongozi wa dini anayefanya kazi kupita kiasi na hufanya kipindi kwa mwaka kuhusu vitu vyote vya gharama anavyopenda.

"Ni kiongozi wa dini asiyechagua kanisa lipi aende. Ni mwanamke anayeteta wazazi wa kike na desturi za kifamilia lakini binfasi hana watoto."

Utata huu unavutia wanawake, alisema." Wanashukuru kwamba wanaweza kumwangalia Oprah na kuona mtu kama rafiki yao wa karibu lakini pia huwapa nafasi katika ulimwengu huu mzuri."