NATO imeshambulia nyumba ya Gaddafi

NATO inasema kuwa imeangamiza minara ya walinzi katika eneo la nyumba ya Kanali Gaddafi wa Libya mjini Tripoli, kwa mashambulio mawili yaliyofanywa na ndege za umoja huo wa kijeshi.

Haki miliki ya picha Reuters

Waandishi wa habari mjini Tripoli, wanasema shambulio moja lilofanywa mchana, lilivunja sehemu za ukuta unaozunguka jengo la jeshi la Bab al-Aziziya.

Msemaji wa NATO, alieleza kuwa shambulio hilo ni funzo kubwa kwa kiongozi wa Libya, kwamba hawezi tena kujificha nyuma ya kuta ndefu.