England: uchaguzi FIFA uahirishwe

Bw. Blatter hana mpinzani Haki miliki ya picha AP
Image caption Sepp Blatter Rais wa FIFA na mgombea pekee

Vyama vya soka katika England na Scotland vimeitaka FIFA iahirishe uchaguzi wa Rais wa shirikisho hilo.

Rais wa sasa Sepp Blatter ndie mgombea pekee wa uchaguzi huo wa Juni mosi baada ya kujiondowa kwa Mohamed Bin Hammam.

Chama cha soka cha England(FA) sasa kinataka uchaguzi uahirishwe na jopo huru liteuliwe ili kupendekeza mfumo wa utawala katika FIFA uboreshwe .

Na taarifa ya chama cha mpira cha Scotland (SFA ) imesema uchaguzi huo uahirishwe" ili kufanikisha kipindi cha mashauriano."

Hata hivyo wachambuzi wa michezo wanasema hatua hiyo ya dakika ya mwisho ya chama cha soka cha England huenda isifue dafu.

Chama cha soka cha England hivi majuzi kiliamua kwamba hakitashiriki katika upigaji kura baada ya kutolewa tuhuma za rushwa na ufisadi dhidi ya Mamlaka ya kusimamia soka duniani..