Sepp Blatter kuendelea kuwa rais wa Fifa

Sepp Blatter Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Sepp Blatter

Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa Sepp Blatter anatarajiwa kushinda muhula wake wanne baada ya wale waliotaka kuahirishwa kwa uchaguzi huo kushindwa kusimamisha.

Mwanamfalme wa Uingereza William ameunga mkono msimamo wa shirikisho la soka la England na lile la Scotland kuwa uchaguzi wa huru na haki hauwezi kufanyika huku kukiwa na madaia ya ufisadi.

Blatter ndiye mgombea pekee kwa kuwa mpinzani wake Mohammed bin Hammam amesimamishwa.

Wakati huo huo, Chuck Blazer,katibu mkuu wa shirikisho la soka la Concacaf, amenusurika kutimuliwa kama katibu mkuu.

Madai ya ufisadi ya Blazer yamesababisha wajumbe wawili wakuu,akiwemo Mohammed bin Hamman, kusimamishwa kuhudumu katika shirikisho hilo.

Mashirikisho ya FA na SFA yamejaribu kutafutwa kuungwa mkono katika pendekezo lao la kutaka uchaguzi kusitishwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa FIFA waliosimamishwa kazi

Mashirikisho mengine kutoka Uingereza,ikiwemo shirikisho la Wales na lile la Ireland,yanaonekana hayako tayari kuunga mkono majirani zao.

Ili kuweza kusitisha uchaguzi wa Jumatano,inahitaji mataifa 150 kati ya 208 kupiga kura kuunga mkono hatua hio,jambo ambalo mwenyekiti wa shirikisho la FA David Bernstein haoni likiwezekana.

Na kwa kuwa tayari wameamua kutoshiriki katika upigaji kura, Bernstein amesema ni muhimu kwa FA kuweka msimamo wake wazi.

''Nafkiri ilikuwa muhimu kwa mtu kusimama kidete na kuchukua msimamo," Aliambia BBC. "kuna suala la maadili hapa na ni muhimu hata kama watu wengine hawafanyi hivyo,FA ichukue uongozi kwa hili.