'Fedha zaidi zahitajika' kwa tiba ya HIV

Haki miliki ya picha
Image caption Muundo wa HIV

Mkuu wa jumuiya ya kimataifa ya ukimwi alisema, uwekezaji zaidi unahitajika wa kupata tiba ya HIV.

Bertrand Audoin amekiri hatua ya kupata tiba inaweza kuchukua zaidi ya miaka 25, lakini amesema tiba ni njia pekee ya kupambana na ugonjwa huo kama njia ya muda mrefu hasa wakati wa msukosuko wa fedha.

Baadhi ya wataalamu wameonya kuwa mazungumzo ya tiba yanaweza kuleta matumaini yasiyo ya kweli, na kutengeneza chanjo ndio itakuwa njia bora.

Bw Audoin alisema: "Ni wakati muafaka- kulingana na mwelekeo wa kisayansi na kifedha- kuwekeza muda zaidi na fedha katika kufanyia utafiti tiba hiyo.

" Tayari utafiti wa kisayansi wa awali ushafanyika kwenye nyanja hii. Tunajua kuna baadhi ya watu wako kwenye matibabu ya HIV ambao wanaweza kuzuia virusi hivyo kwa namna ambavyo hawamwambukizi mtu mwengine.

"Kwahiyo tunadhani utafiti zaidi unaweza kutusaidia kupata tiba ya kudumu, itakayofanya virusi hiyo kubaki mwilini katika hali ya kujificha, bila ya mtu kujisikia anaumwa au kuhitaji tiba. Hiyo ndio lengo."