Balozi wa Nigeria 'ampiga' mkewe Kenya

Nigeria Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ramani ya Nigeria

Serikali ya Nigeria imemuagiza balozi wake nchini Kenya kurudi nyumbani kufuatia madai kuwa alimpiga na kumuumiza mke wake.

Serikali ya Nigeria imesema balozi huyo, Dr Chijioke Wigwe, alitakiwa kurudi nyumbani kama sehemu ya uchunguzi wa madai dhidi yake.

Balozi huyo ana kinga ya kidiplomasia kwa hivyo hawezi kushtakiwa wala kukamatwa nchini Kenya.

Balozi huyo amekanusha madai dhidi yake.