Owen kuichezea Man U kwa mwaka mmoja

Owen
Image caption Michael Owen

Michael Owen ametia saini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Manchester United.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye mkataba wake ulikuwa unamalizika, ameonesha nia ya kutaka kuendelea kusalia Old Trafford.

"Nimefurahi kubakia kwa mwaka mmoja zaidi. Nawashukuru wote kwa kunitumia ujumbe," alisema Owen kupitia mtandao wa Twitter.

Karibu msimu wote uliopita Owen alikaa benchi akiwa manchester United, huku Wayne Rooney na Javier Hernandez na Dimitar Berbatov wakipewa kipaumbele zaidi kucheza.

Alikuwa mchezaji wa akiba katika mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Barcelona. Amecheza mechi 17 katika msimu wa 2010/2011 na kufunga mabao matano.