Hillary Clinton anazuru Afrika

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, ameonyesha wasi wasi juu ya kukua kwa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Uchina na Africa.

Haki miliki ya picha AP

Akizungumza nchini Zambia, Bi Clinton alisema msaada wa nje wa Uchina na uwekezaji wake barani Afrika haujakidhi viwango vya kimataifa vya uwazi na utawala bora, na wala haujawahi kutumia vipaji vya Waafrika katika kutafuta maslahi ya kibiashara ya Uchina.

Bi Clinton alihimiza kuwepo kwa mkataba wa kibiashara ambao utaipatia Afrika nafasi ya kusafirisha bidhaa bila ushuru kwenye masoko ya Marekani, huku akiwasisitizia viongozi wa Africa, kuondoa vikwazo vya kibiashara katika mataifa yao na kupambana na ufisadi.

Bi Clinton anatembelea nchi tano, na Jumapili anatarajiwa kuwasili Tanzania.