Gaidi maarufu auwawa Pakistan

Taarifa kutoka Waziristan Kusini zinaonesha kuwa mpiganaji wa daraja ya juu wa Pakistan, Ilyas Kashmiri, aliuliwa jana usiku katika shambulio la ndege ya Marekani, isiyokuwa na rubani.

Haki miliki ya picha AP

Ilyas Kashmiri alikuwa kiongozi wa Harkatul Jihan al-Islami, kikundi cha msimamo mkali kinachoshirikiana sana na al-Qaeda.

Ametuhumiwa kuhusika na mashambulio mengi pamoja na shambulio maarufu la karibuni, dhidi ya kituo cha jeshi la wanamaji la Pakistan, mjini Karachi.

Piya alihusishwa na mashambulio ya Mumbai miaka mitatu iliyopita.

Mwandishi wa BBC mjini Islamabad anasema taarifa kuhusu kifo cha Ilyas Kashmiri, zitapokelewa uzuri na serikali ya Marekani, ambayo inamhusishwa na mashambulio nchini Afghanistan piya.

Marekani ilitangaza bahashishi ya dola milioni 5 kwa yeyeto atayewajulisha gaidi huyo aliko.