Makanisa ya Sudan yanalaani mapigano

Baraza la makanisa ya Sudan linasema lina wasiwasi mkubwa juu ya mauaji makubwa ya raia katika majimbo ya Abyei na Kordofan Kusini.

Haki miliki ya picha Reuters

Katika taarifa yake, baraza hilo linasema watu wameuwawa bila ya kufikishwa mahakamani.

Majimbo hayo kwenye mpaka baina ya Sudan Kusini na Kaskazini, hivi karibuni yamekumbwa na mapigano baina ya jeshi la kaskazini, la kusini na makundi mengine.

Makanisa yameulaumu Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuwalinda raia, na yamezilaani serikali za kaskazini na kusini Sudan, kwa kutumia nguvu kutatua hitilafu baina yao.