Wanasayansi watafuta chanzo cha E-coli

E-coli Haki miliki ya picha JP
Image caption E-coli

Wanasayansi wanaojaribu kutafuta chanzo cha mdudu wa bacteria wa aina ya E-coli, aliyeuwa watu kama 18, na kuambukiza mamia kadha.

Wanachunguza mkahawa kaskazini mwa Ujerumani.

Watu 17 waliumwa baada ya kula katika mkahawa huo, katika mji wa L├╝beck.

Maafisa wa afya piya wanachunguza vibanda vilivokuwa vinauza chakula katika tamasha iliyohudhuriwa na watu kama milioni moja na nusu katika bandari ya mji wa Hamburg, kati ya mwezi uliopita.

Ikiwa wakuu watatambua vibanda vilivouza chakula kilichoathirika, basi wanaweza kuchunguza asili ya chakula hicho.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii