Waandamanaji wafyatuliwa risasi Golan

Waandamanaji mpakani mwa Syria na Israel Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji mpakani mwa Syria na Israel

Wanajeshi wa Israel wamewafyatulia risasi waandamanaji wanaowaunga mkono Wapalestina, kuwazuwia wasivuke mpaka wa Syria, kuingia katika eneo la milima ya Golan, linalokaliwa na Israel.

Waandamanaji kadha walionekana wakibebwa; na kuna taarifa zisizothibitishwa kuwa kama wanne wameuwawa.

Israel ilesema itazuwia maandamano hayo yasiwe kama yale yaliyotokea mwezi uliopita, ambapo watu zaidi ya 10 waliuwawa.

Leo ni siku ya kukumbuka kuanza kwa vita vya siku 6, vya mwaka wa 1967, ambapo Israel ililiteka eneo la Golan.