Wareno wapiga kura katika uchaguzi

Wagombea Coelho na Socrates Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wagombea Coelho na Socrates

Watu wa Ureno wanapiga kura katika uchaguzi ulioitshwa mapema, baada ya serikali ya kisoshalisti, kuomba mikopo kutoka vyombo vya fedha vya kimataifa, kusaidia uchumi wa nchi hiyo.

Kampeni ya uchaguzi imegubikwa na sera za kukata matumizi na kuzidisha kodi, shuruti iliyopewa Urenu ili kupata msaada.

Kura za maoni zinaonesha mashindano ni makali baina ya chama tawala cha kisoshalisti, na cha mrengo wa kati, cha Social Democrats.

Mwandishi wa BBC, anasema yeyote atayeshinda uchaguzi, atakuwa na tatizo kubwa la kutekeleza sera hizo.